Tuesday, November 13, 2012

Wanafunzi Wa Mkoa Wa Dar-es-Salaam Chini Ya Tafes Waadhimisha Wiki la Uinjilisti Pamoja

Wanafunzi wa Elimu Ya Juu Katika Vyuo Mbalimbali Katika Mkoa wa Dar-es-Salaam walio chini ya affiliation ya TAFES wamehitimisha wiki la Uinjilisti kwa kufanya Ibada Maalum katika Kanisa la DPC lililo Dar-es-Salaam.
Katika Ibada hiyo iliyoanza majira ya saa 8 Mchana na Kuhudhuriwa na Wanafunzi, Tafes Staff, Associates na Watumishi wengine ilikuwa ya aina yake siku ya jana. Pastor Safari pamoja na Rivers Of Life ndio walioongoza Praise and Worship kwa siku ya Jana.

Pastor Carlos kama ilivyo ada ya Karama yake ya Ualimu alifundisha namna ya kuwafikia wengine kupitia kubadilishwa kwako kupitia neno. Akifundisha katika Jioni ya Jana Pastor Carlos alisema "You cant live a life of impact, without being impacted kwanza, huwezi kuwafikia wengine kabla wewe mwenyewe hujafikiwa kwanza, ni lazima neno liwe limefanya jambo kwenye maisha yako ndipo utakapoweza kutenda jambo kwa wengine"Tafes ni Organization inayofanya Kazi na wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu hapa Tanzania kwa Kuwafikia kwa neno la Mungu na Kuwafundisha kwa ajili ya maisha ya Utauwa na Ucha Mungu. Tafes haipo chini ya dhehebu fulani ni Interdenominational Organisation.

Pia katika Siku ya Jana alikuwepo Director wa Tafes Tanzania, Mr. Rex, Alikuwepo Makamu Mwenyekiti wa Board Mr. Ben na Pia alikuwepo Mwenyekiti wa Tafes Mkoa wa Dar-es-Salaam Mr. Simalenga.



 Inter Collage Praise Team Ikihudumu siku ya Jana Ndani ya DPC




 Twende Kazi




 Kulia Viongozi wa Taifa na Mkoa wakiwa kwenye Ibada




 Wanafunzi ndani ya DPC




 Pastor Carlos akishusha nondo




 Twende Kazi Jembe




 Amepona kabisa Mguu kwa sasa




 Ze Blogger Ndani ya Tafes

No comments:

Post a Comment