Sunday, December 2, 2012

DKT HURUMA NKONE NA USCF MLIMANI WAOMBEA TAIFA NA MCHAKATO WA UANDISHI WA KATIBA MPYA KWA MZIGO SANA

Ilikuwa ni siku ya Jumamosi, tar 01 Disemba, kuanzia saa 1 mpaka 3 usiku, Mch. Dkt. Huruma Nkone aliongoza maombi yenye nguvu ya kuombea mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya na Taifa kwa ujumla. Vijana na wanataaluma hao wa Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam chini Umoja wao uitwao University Students Christian Fellowship(USCF)-MLIMANI chini ya Jeremiah Juma (Mwenyekiti) na Joshua Shoo(Katibu), walipaza sauti zao na kuombea jambo hilo muhimu sana kwa mstakabari wa Taifa letu.

Mch. Dkt. Huruma Nkone 

Mwenyekiti (Jeremiah Juma)-kushoto na Katibu (Joshua Shoo)

Dkt Huruma Nkone, mpenzi wa wasomi na watu wote wenye nia ya kuwa wakuu katika Kristo Yesu na aliyeambatana na jeshi la vijana toka Victory Christian Centre Tabernacle; Samwel Fred , Prosper Mwakitalima, Irene Lyatuu, Eunice Kahogo na Bw. Gerson Fungo, baada ya kusoma “Zaburi 33:12” alianza kwa kufafanua kwanini twahitaji kuombea mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya na Taifa.


Aliyataja mambo kadhaa ya kuombea ikiwamo; 1.Kujiweka wakfu kwa kutubu ili Bwana ayapokee maombi yetu. 2. Kuombea watu wote wanaotoa maoni; kama walioandika Biblia walivuviwa wasiandike mawazo yao ila kile Mungu alitaka, hata Babu wa kijijini anaweza kutoa mawazo mazuri yakulipeleka Taifa katika njia sahihi. 3. Kuiombea Tume ya ukusanyaji maoni ya wananchi. 4. Kuombea mchakato mzima usiingiliwe na dosari yeyote; wenye nia zao mbaya washindwe na kusudi la Bwana litimie. n.k.  
Ukumbi mzima ukamwomba Kristo Yesu ahusike  
Wito kwa wenye nia njema ni kuendelea kuombea mchakato huo ikiwa ni pamoja kwenda kutoa maoni kupitia njia mbalimbali ambazo tume imetoa kurahisisha ukusanyaji maoni ili Taifa hili lisiingie katika matatizo kwa matakwa ya watu wachache. INAWEZEKANA NA BWANA YESU YU PAMOJA NASI.     

Mratibu wa  maombi (Abigael Nkindwa) akamwita akamsihi Bwana

Mama Mkubwa (Bernadetta Kasase)-kulia  na Mama Mdogo (Beatrice Isaya)-katikati wamezama;

Prosper Mwakitalima; Director wa CAMPUS MINISTRY, VCCT, naye aliitia jina la Mnazareth Yesu

Mwanasheria, Mtumishi wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Irene Lyatuu-kushoto, akamlingana Bwana

Eunice Kahogo-katikati; Coordinator CAMPUS MINISTRY,VCCT, aombea Katiba Mpya

Namna hii lazima Bwana asikie kilio cha watumishi wake. Huyu ni Emmanuel Kashishila


Bw Gerson Fungo akashiriki kikamilifu


Msomi mwingine akiomba Katiba mpya toka kwa Bwana na si wajanja wachache

Kila mtu kwa staili yake, bora tu Bwana apokee dua za watu wake kwa ajili ya Tanzania