Ile baada maalum ya kuweka wakfu wanafunzi wa vyuo vikuu kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo ambayo iliandaliwa na Kanisa la Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) linaloongozwa na Mch. Dr. Huruma Nkone chini ya Idara ya Wanafunzi (Campus Ministry) imekuwa ya aina yake na ya kipekee. wanafunzi toka kila kona ya jiji la Dar es salaam walikusanyika katika kanisa la VCCT lililopo Mbezi A jijini Dar es salaam
Kwaya na vikundi mbali mbali vilikuwepo kumtukuza Mungu katika siku hii. miongoni mwa vikundi vilivyo hudumu ni Mabibo Christian Fellowship Choir toka UDMCF, Kwaya ya CASFETA Dar es salaam, Kwaya toka Chuo cha DIT, Kwaya toka Ardhi University (TAFES Praise team) na Kundi la Glorious Worship Team (GWT) bila kusahau watoto wa nyumba ya VCCT The Rivers of Joy International (RoJI).
Ibada hii ya shangwe iliongozwa na Dr. Huruma Nkone na kuratibiwa na Idara ya wanafunzi (Campus Ministry).
Katika siku hii wanafunzi wa vyuo walipata fursa ya kusikiliza neno toka kwa Mch. Dr. Nkone, na baada ya hapo, Dr. Nkone alifanya maombi maalum kwa ajili ya wanafunzi kwa ajili ya kuwaweka wakfu kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo, na baada ya ibada Dr. Nkone alikutana na wanafunzi hao kwenye eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili yao na kupata soda pamoja na wanafunzi hao na kisha kuomba baaraka kwa ajili yao.
Tukio la kupiga picha lilifuata ambapo viongozi wa fellowship walipata fursa ya kupiga picha na Mchungaji Dr. Nkone katika red carpet iliyoandaliwa kwa ajili yao.
 |
Moderator 1st service, CEO wa MANCON EA LTD, Brother Pro
|
 |
DIT Choir wakimtuza MUngu |
 |
watu wakienda sawa |
 |
The Bomby, Fredy Msungu na Amani Kapama wakifanya kweli |
 |
Ardhi University Tafes Praise team |
 |
Campus Ministry team na Dr. Nkone |
 |
Kairuki University Pamoja na Mch DR. Nkone |
 |
Pokeaaaa kwa Jina la Yesu Kristo |
 |
UDMCF Praise team wakiimba
|
 |
RoJI watoto wa Nyumbani wakiimba
More Pictures to Come.............
|