Sunday, December 30, 2012

KONGAMANO LA KIPEKEE KABISA LA KITAIFA LA CASFETA LAFANYIKA


Mchungaji Dkt Huruma Nkone, Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Victory Christian Centre Tabernacle, pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya wanafunzi wa shule, vyuo na vyuo vikuu waliookoka  ya CASFETA. 

Akishilikiana na jopo la viongozi wake waliandaa kongamano la kipekee sana la viongozi na wanafunzi wote kama ilivyo kawaida kwa kila mwezi Desemba. Zilikuwa siku mbili zenye nguvu sana, tar 18 na 19 Desemba baada ya watu kuwasili kambini tar 17 pale zaidi ya wana-CASFETA 1000 walipokusanyika katika Shule ya St. Cornelius High School, Salasala, Tegeta, Dar-Es-Salaam. Walipata mafundisho, kufanyiwa maombezi na kuandaliwa kwa kazi kubwa ya kujenga chombo hicho, kanisa na Taifa kwa ujumla.

Kingine kikubwa ni kuwa, Mwaka huu 2012, CASFETA imesherehekea MIAKA 20 tangu kuanzishwa kwake (20th Anniversarry)

Ukumbi ukiwa umefurika; Maombezi yakiendelea 

Mkurugenzi Mkuu, Mch Dkt Huruma Nkone  

 Makamu Mkurugenzi Mkuu, Mch Weston Sambo

Katibu Mkuu, Bi Florence Mbago  

Kelvin Ngonyani; Mwenyekiti wa CASFETA wa Taifa wa wanafunzi(RAISI); Mwanafunzi wa SUA

Mch Dkt Huruma Nkone (Katikati), Bi. Florence Mbago(Kushoto) & Mch Weston Sambo(Kulia)

Maombi yanaendelea kufanyika. Kizazi kiletacho mabadiliko chaandaliwa

CASFETA ASSOCIATE, Ev Gregory Daudi (kushoto) akiwa na Mch Dkt Huruma Nkone 

Mkurugenzi wa CASFETA Kinondoni, Dkt Dickson Mkoka

Rose Mushi

Mch Julius Mkenda (katikati) na Mkewe (Bi Haika Mkenda) wakipokea toka kwa Mkurugenzi CASFETA


Katibu Mkuu, Bi Florence Mbago alikuja na mmewe, Bw Lucas Mbago (katikati)

Wana CASFETA wakiwa makini mafundisho yanapotolewa

Dar Praise & Worship Team wakaimba wimbo wa shukrani kwa Mungu kwa Miaka Ishirini ya CASFETA

John Lisu akaongoza sherehe za kumsifu Mungu kwa Miaka ishirini ya CASFETA

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo wakiachilia baraka kwa wadogo zao ili wafike vyuo vikuu

Kila pando la Ibilisi lang'olewa, Bwana anapanda kitu ndani ya binti huyu; Hakika Taifa linaenda kupona

Kila pando la Ibilisi lang'olewa, Bwana anapanda kitu ndani ya binti huyu; Hakika Taifa linaenda kupona

Hawa ni sehemu ya  wanaCASFETA waliohudhuria kongamano