Tuesday, February 4, 2014

"MWAKA WA KAZI" IFM TAFES & TAFES ARDHI WAPEWA SUPPORT KUFANIKISHA MISSION TRIPS ZAO

Ni ukweli usiopingika kwamba "You can't Separate VCCT and Students". Kanisa hili limekuwa vinara wa kufanya kazi na wanafunzi wa vyuo vikuu katika kupeleka injili ya Yesu Kristo katika jamii za watu wasiofikiwa na injili iyo.

Katika kuendeleza hayo wiki hii, kanisa la VCCT lilitoa sadaka maalum ya Upendo " A love Offering" kwa ajili ya kusoport kazi ya wanafunzi wa vyuo viwili hapa Dar es salaam ambao wanajiandaa kwenda missions mwishoni mwa wiki hii.

Vyuo ambavyo vilinufaika na sadaka iyo ni IFM ambao wenyewe wanakwenda mission mkoa wa Tanga, Mkinga District, Maramba Village. wakati Ardhi University wanakwenda Mkoa wa Njombe.

Akikabidhi sadaka iyo kwa niaba ya Mch. Kiongozi Dr. Huruma Nkone, Mkurugenzi wa Campus Ministry Mr(Dr.) Samuel Sasali amewataka wanafunzi hao wajisikie nyumbani, any time they think they need us wasisite kutuona. Aliwakabidhi sadaka izo pamoja na nguo na vitu mbali mabaloi ambavyo watakwenda kuwabariki watu wa huko na kuwatakia utumishi mwema.


IFM praise Team




Ardhi team


All the best IFM


All the best Ardhi university






Sunday, February 2, 2014

VCCT WACHANGIA SAFARI YA MISSION YA WANAFUNZI WA UDSM

Kanisa la VCCT wiki iliyopita ilichangia kiasi cha zaidi laki 8, kusaidia safari ya kimisheni wa wanafunzi wa UDSM  Christian Fellowship,

Akikabidhi sadaka iyo, Mr. Sasali Samuel ambaye ni Director wa Campus Ministry, kwa niaba ya Mch. Dr. Huruma Nkone, alisema " Mioyo yetu ipo kwa ajili ya wanafunzi, na Tutakuwa tayari kuwasidia muda wowote, msiache kuja"

Kabla ya kukabidhi Sadaka iyo, wanafunzi hao walipata Fursa ya kuimba katika Ibada wakati washirika wa VCCT walipoikuwa wakitoa sdaka iyo

UDSM choir singing

The Choir

CM Leadership With UDSM Fellowship leadership


Mr. (Dr.) Samuel Sasali akikabidhi sadaka iyo