Tuesday, January 22, 2013

UINJILISTI WA WANAFUNZI WA VYUO VIJIJINI (MISSION)


Huduma ya injili ni moja ya mabo wanayofanya wanafunzi waliiokoka mbali na masomo. Hufanya uinjilist kwa wanafunzi wenzao ambao hawajamjua Kristo na pia kwenda maeneo ya vijijini ambako injili haijafika kabisa au imefika kwa kiwangi kidogo.
Baadhi ya vyuo ambavyo vinatazamia kupeleka injili sawasawa na neno la Mungu katika Mathayo 28:19 (Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu).

Program ambazo hufanywa huko ni pamoja na;
Mkutano wa nje (crusade)
Uinjilist nyumba kwa nyumba (door to door) na mtu kwa mtu, wengine pia huwa na shamba kwa shamba
Ukarimu (charity) kama vile kugawa nguo, vifaa vya shule n.k
Mahubiri kwa njia ya Cinema pamoja na huduma zingine mbalimbali.

Baadhi ya vyuo vinavyotarajia kwenda kwa mwaka huu wa masomo ni pamoja na;

ARDHI--TAFES, 2-9, Feb wanaenda Mtwara kijiji cha Nanyamba. Idadi ya wanafunzi wanaotazamia kwenda ni zaidi ya 110.

                               Hawa ni wainjilisti watakaokuwa wakisimama madhabahuni kuongoza mashambulizi juu ya falme za giza, kuuteka ufalme ulioibiwa na mwovu ibilisi


ARDHI--CASFETA TAYOMI, 4-11, Feb, wanaenda Tanga- Kiomoni. Idadi ya watakaopeleka injili huko ni zaid ya wanafunzi 50.

Wana CASFETA ARDHI praise team wakiongoza wengine katika kusifu katika Roho na kweli

CASFETA Praise team wakihudumu kwenye mkutano wa nje katika moja ya mission


CASFETA  UDSM , Wataenda Chole Samvula, Pwani,  3-10 Februari.


Wengine wanaotazamia kwenda semister ijayo ni;

DIT- Kilimanjaro, July

UDSM-USCF-Rukwa, wanatarajia kwenda mwezi June

UDSM- MCF Morogoro-Ifakara, July