Wednesday, December 26, 2012

CHRISTMAS PRODUCTION YAFANA NDANI YA VCCT

Moja ya matamasha makubwa yanayochukua nafasi hapa jijini Dar, Christmas Production inaendelea kufana. Tukio hili hufanyika kila tar 26 Disemba 2012, siku moja baada ya siku Mwokozi wetu Yesu Kristo alipozaliwa. Ninapoandika,  tukio hili linaendelea na watu wanamsifu na kumwabudu Mungu kwa namna nisiyoweza elezea. Ndani ya nyumba wapo Rivers of Joy International, Glorious Celebration, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Amani Isayah, Bomby Johnson, Samuel Yonah, President Chavala, Mc Pilipili, CASFETA Dar P & W team.   


         Mch. Dkt Huruma Nkone, Mchungaji Kiongozi na mbeba maono 

                                                                       Mch Joyce Nkone
Ukumbi umefurika; watu wanamsifu aliyezaliwa 


 Upendo Nkone


 Upendo Kilahiro

MC...Samuel Sasali


Glorious Celebration; wametuabudisha na wao wanaabudu

 Upendo Nkone naye anaabudu


MC.. Pilipili na  Chris Mauki


Ada, aina ya Upendo Nkone mwingine anayejitokezea


Vijana chipukizi, ROJI  junior wa VCCT



Watumishi wa Mungu M Timothy Kyara na mkewe; UK & TANZANIA

Upendo Kilahiro & Mpelo Kapama, Kiongozi wa Muziki na Uimbaji, VCCT


Mc & President  Chavala


Bw Hillary Samwel (Kushoto) na Bw Misericodius (kushoto) wakimtukuza Mungu



Ukumbi haukutosha. Na watoto nao hawakubaki nyumbani; walikuwepo.

Naomi Venance; Binti aliyebarikiwa kiuimbaji. Toka UDSM, Mtoto wa VCCT.

Rivers Of Joy International; Wakiongoza umati mkubwa sana wa watu Kumsifu Mungu

Sunday, December 2, 2012

DKT HURUMA NKONE NA USCF MLIMANI WAOMBEA TAIFA NA MCHAKATO WA UANDISHI WA KATIBA MPYA KWA MZIGO SANA

Ilikuwa ni siku ya Jumamosi, tar 01 Disemba, kuanzia saa 1 mpaka 3 usiku, Mch. Dkt. Huruma Nkone aliongoza maombi yenye nguvu ya kuombea mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya na Taifa kwa ujumla. Vijana na wanataaluma hao wa Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam chini Umoja wao uitwao University Students Christian Fellowship(USCF)-MLIMANI chini ya Jeremiah Juma (Mwenyekiti) na Joshua Shoo(Katibu), walipaza sauti zao na kuombea jambo hilo muhimu sana kwa mstakabari wa Taifa letu.

Mch. Dkt. Huruma Nkone 

Mwenyekiti (Jeremiah Juma)-kushoto na Katibu (Joshua Shoo)

Dkt Huruma Nkone, mpenzi wa wasomi na watu wote wenye nia ya kuwa wakuu katika Kristo Yesu na aliyeambatana na jeshi la vijana toka Victory Christian Centre Tabernacle; Samwel Fred , Prosper Mwakitalima, Irene Lyatuu, Eunice Kahogo na Bw. Gerson Fungo, baada ya kusoma “Zaburi 33:12” alianza kwa kufafanua kwanini twahitaji kuombea mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya na Taifa.


Aliyataja mambo kadhaa ya kuombea ikiwamo; 1.Kujiweka wakfu kwa kutubu ili Bwana ayapokee maombi yetu. 2. Kuombea watu wote wanaotoa maoni; kama walioandika Biblia walivuviwa wasiandike mawazo yao ila kile Mungu alitaka, hata Babu wa kijijini anaweza kutoa mawazo mazuri yakulipeleka Taifa katika njia sahihi. 3. Kuiombea Tume ya ukusanyaji maoni ya wananchi. 4. Kuombea mchakato mzima usiingiliwe na dosari yeyote; wenye nia zao mbaya washindwe na kusudi la Bwana litimie. n.k.  
Ukumbi mzima ukamwomba Kristo Yesu ahusike  
Wito kwa wenye nia njema ni kuendelea kuombea mchakato huo ikiwa ni pamoja kwenda kutoa maoni kupitia njia mbalimbali ambazo tume imetoa kurahisisha ukusanyaji maoni ili Taifa hili lisiingie katika matatizo kwa matakwa ya watu wachache. INAWEZEKANA NA BWANA YESU YU PAMOJA NASI.     

Mratibu wa  maombi (Abigael Nkindwa) akamwita akamsihi Bwana

Mama Mkubwa (Bernadetta Kasase)-kulia  na Mama Mdogo (Beatrice Isaya)-katikati wamezama;

Prosper Mwakitalima; Director wa CAMPUS MINISTRY, VCCT, naye aliitia jina la Mnazareth Yesu

Mwanasheria, Mtumishi wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Irene Lyatuu-kushoto, akamlingana Bwana

Eunice Kahogo-katikati; Coordinator CAMPUS MINISTRY,VCCT, aombea Katiba Mpya

Namna hii lazima Bwana asikie kilio cha watumishi wake. Huyu ni Emmanuel Kashishila


Bw Gerson Fungo akashiriki kikamilifu


Msomi mwingine akiomba Katiba mpya toka kwa Bwana na si wajanja wachache

Kila mtu kwa staili yake, bora tu Bwana apokee dua za watu wake kwa ajili ya Tanzania

Tuesday, November 20, 2012

Campus Night In Mbeya ni Next Next Level

Katika Weekend hii Big Events za wanafunzi zenye jina La Campus Night zimechukua mkondo wake katika mikoa ya Dodoma na Mbeya.

Blogger akiripoti kutoka Mbeya ameeleza kuwa Campus Night ya Mbeya imevunja Records ya Makusanyiko ya vijana na wanafunzi katika jiji hilo, event hiyo iliyokusanya wanafunzi zaidi ya 7000 ilikuwa na theme ya Raising The Standards.
Mwimbaji wa Injili anayevuma na ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu mkoani humo Ambwene Mwansongwe ndiye aliyeteka ukumbi kila aliposimama.
Wachekeshaji wanaovuma katika tasnia ya Gospel, King Chavalla na Mc Pilipili walinogesha Campus night yaJiji la Mbeya.
Wanenaji Wakuu Katika Usiku huo Dr. Huruma Nkone, Dr. Kimambo, Ms Rose Mushi na Mr. Msigwa wali Raise Standards za Wanafunzi.

Dr. Huruma Nkone aliyekuwa akifundusha Spiritual Transformation usiku huo alilipuka kinjilisti na kuwaambia wanafunzi 'Usharubalo na Utoz Toz,hautainua kiwango chako cha Kiroho, isipikuwa kwa kumpokea Yesu' akinukuu andiko la kutoka kwenye kitabu cha Yohana ikisema 'Mimi ndimi njia kweli na uzima, mtu haendi kwa Baba Isipokuwa kwa njia ya Mimi"
Dr. Kimambo alifundisha Academic and Career Challenges zinazowakabili wanafunzi.Dr. Kimambo ambaye ni Mwajiriwa wa Serikali yaUingereza nchini Tanzania alieleza 'changamoto za mfumo wa elimu na mahitaji ya soko la ajira ni tatizo linalo wakabili wanafunzi. Tatizo la Soft Skills mbali na ule ujuzi unaopatikana vyuoni ni changamoto pia.Mbali na changamoto hizo maendeleo na matumizi ya technolojia katika mfumo globalization ni changamoto inayowakabili wahitimu wa Elimu Ya Juu.
Mwanadada aliyekuwa msemaji pekee katika Campus night na mdogo wa umri kuliko wasemaji wote Dada Rose Mushi alifundisha RaisingThe Standard Of Ladies In the Campus. Rose Mushi ambaye ni Mchumi kwa taaluma na mwajiriwa wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Aliamsha hamasa kubwa ya vijana alipoanza kufundisha kutoka kwenye Kitabu Cha Mwanzo kwenye story ya Yusufu na Mke wa Potifa. Akifundisha Usiku huo Rose Mushi alisema ili kuinua Viwango vya Kiroho Vya Akina dada katika Campus inapaswa kwanza Ujue thamani yako kama Mdada, pili inakupasa kuachana na mambo yote ambayo yanakusababishia kukushikilia kwa mwanaume kama mi kufaulu, kama ni ada, kama ni laptop kama ambavyo Yusufu alimwachia vazi Mke wa Potifa.
Somo la Mahusiano lilifundishwa na Mr. Msigwa Meneja wa tawi la CRDB katika wilaya ya Mbozi. Alieleza uhusiano wowote wa mwanaume na mwanamke hauwezi kuwa mzuri kama wahusika wana uhusiano mbaya na Mungu wao.
Praise and Worship Leaders. Mr and Mrs Matthew Sasali

Event hiyo ilisimamiwa na Dr. Nyanda pamoja na Ze Blogger. Praise Team ilisimamiwa na Pastor Matthew Sasali na Rebecca Sasali
Dr. Nyanda, Rose Mushi na Papaa Ze Blogger hapo ilikuwa saa 1 Asubuhi baada ya event.

Matukio Katika Picha.
 Sehemu Ya Umati Wa watu
 Mrs. Rebecca Sasali akiongoza Praise Team
 Wanafunzi Waliotoka Mbele Kumpa Yesu Maisha Yao Zaidi ya wanafuzi 90 walimpa Yesu Maisha yao.
 Ndani Ya Uwepo
 Watu Wakienda Sawa ndani ya Ukumbi
 Full Shangwe Wanafunzi Wa Mbeya
 Chezea Nyomi
 Respected Event Manager Papaa Ze Blogger ndani ya Ukumbi
 Ukumbi Mzima Kidole namba tatuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 Watu Wakimpa Yesu Maisha Yao.
 Rose Moshi Kikazi zaidi
 Chezea Urefu
 Wakienda sawa
 Huu Mwili Khaaaa
 Pilipili Kikazi Zaidi ndani ya Mbeya
 Kikazi Zaidi hapa
 Safari Hii akaja na Style ya Sketi aiseeee ilikuwa nouma inaitwa "Usiombe Kusutwa'
 Dr. Maboko akizungumza kwenye Campus Night
 King Chavallaaaaaaaa akienda sawa ndani ya Campus Night
Jamaa kumbe akivua Kofia ni handsome sanaaaaaaaa